MANCHESTER, England
IMERIPOTIWA kuwa mshambuliaji wa Manchester United, Marcus Rashford, atatimkia Barcelona kwa mkataba wa mkopo.
Barca walifika mezani na ofa yao ya mkopo na Man United wameripotiwa kukubali baada ya kumwambia Rashford kuwa hayuko kwenye mipango yao ya msimu ujao.
Taarifa zinaeleza kwamba Wacatalunya hao wamekubali kulipa asilimia 100 ya mshahara wa mchezaji huyo, ambao ni Pauni 325,000 kwa wiki.
Kwa mshahara huo, Man
Barca wanakazania dili hilo likamilike mapema wiki ijayo, kabla ya kikosi chao kwenda ‘pre-season’ barani Asia.
Rashford aliumaliza msimu uliopita akiwa mkopo katika klabu ya Aston Villa.
Kwa sasa, bado Rashford anaonekana katika Uwanja wa Carrington akijifua na wachezaji wenzake wa Man United, wakiwamo Antony na Alejandro Garnacho, ambao pia wanaweza kuondoka majira haya ya kiangazi.
Published:


