LOS ANGELES, Marekani
SUPASTAA wa muziki wa Hip hop, Snoop Dogg, amenunua hisa katika klabu ya Swansea City.
Kwa kufanya hivyo, sasa rapa huyo anakuwa sehemu ya wamiliki wa klabu hiyo, akiungana na kiungo Luka Modric.
Swansea iliyowahi kushiriki na kufanya vizuri katika mikikimikiki ya Ligi Kuu ya England, kwa sasa iko Ligi Daraja la Pili.
Akizungumzia hatua hiyo, Snoop ambaye ni mshindi wa alisema: “Mapenzi yako kwa soka yako wazi lakini najisikia furaha Zaidi kuwa sehemu ya wamiliki wa Swansea City.”
Published:


