RIO, Brazil
BAO la dakika za mwisho la Neymar limeiwezesha Santos kuzoa pointi tatu katika mchezo wao dhidi ya Flamengo, ambao ni wa Ligi Kuu ya Brazil.
Neymar amekuwa kwenye majanga katika miezi ya hivi karibuni, kubwa ikiwa ni mfululizo wa majeraha.
Dhidi ya Flamengo, ilikuwa ni mechi ngumu kwa Santos, ikizingatiwa kuwa wenzao hao walifika hatua ya 16 bora ya Kombe la Dunia kwa ngazi ya Klabu.
Kabla ya kutolewa na vigogo hao wa Ligi Kuu ya Ujerumani, Flamengo waliushangaza ulimwengu wa kandanda kwa kuwafunga Chelsea.
Published:


