CATALUNYA, Hispania
STAA wa Barcelona, Lamine Yamal, anachunguzwa kwa kile alichokifanya wakati wa sherehe ya ‘birthday’ yake ya kutimia umri wa miaka 18.
Katika sherehe hiyo ya hivi karibuni, Yamal alialika watu wenye udumavu kutumbuiza, jambo ambalo sasa linamwingiza matatani.
Waalikwa hawakuruhusiwa kuingia na simu lakini imevuja video ikionesha watu wenye udumavu wakiingia ukumbini.
Sasa, Wizara ya Ustawi wa Jamii ya Hispania imeomba ufanyike uchunguzi ili kubaini sababu ya watu hao kuhudhuria na endapo itabainika walilipwa kwa ajili ya kuburudisha, basi Yamal achukuliwe hatua za kisheria.
Kabla ya agizo la Wizara, tayari Chama cha Wenye Ulevu cha Hispania (ADEE) kililaani vikali tukio hilo.
“Haikubaliki kuona katika karne ya 21, bado watu wenye ulemavu wanachukuliwa kama burudani, hasa kwenye matukio yanahusisha watu maarufu,” alisema Rais wa ADEE, Carolina Puente.
Published:


