ALGER, Algeria
KOCHA mwenye jina kubwa Afrka, Rulani Mokwena, amejiunga na mabingwa wa Ligi Kuu ya Algeria, Mouloudia Alger.
Kwa wiki kadhaa za hivi karibuni, Mokwena mwenye umri wa miaka 38 alikuwa akihusishwa na Orlando Pirates ya Afrika Kusini.
Kabla ya kutimkia Algeria, kocha huyo hakuwa na kazi tangu alipoachana na Wydad Casablanca.
Mokwena aliondoka baada ya msimu mmoja tu uliomalizika wakiwa nafasi ya tatu kwenye msimamo wa Ligi Kuu ya Morocco, pia Wydad ikikosa tiketi ya kushiriki Ligi ya Mabingwa Afrika.
Akiwa Algeria, sasa Mokwena atakutana ana kwa ana na makocha wawili aliowahi kufanya nao kazi Ligi Kuu ya Afrika Kusini.
Makocha hao ni Josef Zinnbauer aliyekuwa Orlando Pirates, ambaye sasa yuko na JS Kabylie, na Sead Ramovic aliyekuwa TS Galaxy na sasa anainoa Chabab Belouizdad.
Published:


