13.9 C
New York

Xhaka kumfuata Lacazette, mshahara bil. 30/-

Published:

RIYADH, Saudia
KIUNGO wa zamani wa Arsenal, Granit Xhaka, amekubali kujiunga na Neom SC ya Saudia akitokea Bayer Leverkusen.
Neom SC ambayo ni timu iliyopanda daraja Ligi Kuu ya Saudia, pia inaye staa wa zamani wa Arsenal, Alexandre Lacazette.
Tangu alipoondoka Arsenal mwaka 2023, Xhaka amecheza mechi 99 akiwa na Leverkusen, akifunga mabao sita na kutoa ‘asisti’ tisa.
Kwa mujibu wa taarifa, Xhaka mwenye umri wa miaka 23 atakunja euro milioni 10 (zaidi ya Sh bil. 30 za Tanzania) kwa mwaka.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img