MILAN, Italia
NI rasmi sasa kiungo wa kimataifa wa Croatia, Luka Modric, ni mali ya vigogo wa Serie A, AC Milan.
Modric mwenye umri wa miaka 38 ametua Milan baada ya misimu 13 ya mafanikio akiwa na Real Madrid.
Milan wamempa mkataba wa mwaka mmoja, ukiwa na kipengele kinachoruhusu kusaini mwingine wa miezi 12.
Nyota huyo alitangaza miezi miwili iliyopita kuwa angeondoka Madrid baada ya kumalizika kwa fainali za Kombe la Dunia kwa ngazi ya Klabu.
Akiwa Madrid, Modric ambaye ni mshindi wa Ballon d’Or mwaka 2018, alitwaa mataji 28.
Alifunga mabao 43 katika mechi 597, ya mwisho ikiwa ni nusu fainali ya Kombe la Dunia ngazi ya Klabu dhidi ya PSG wiki iliyopita.
Published:


