DUBAI, UAE
MAHAKAMA ya Kimataifa ya Uhalifu wa Kivita (ICC) imelaani kinachoendelea mjini Darfur, Sudan, ikieleza kuwa kumekuwa na ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu.
Tangu Aprili, 2023, yamekuwapo mapigano makali kati ya jeshi la Serikali na wanamgambo wa Rapid Support Forces (RSF).
Sasa, uchunguzi wa ICC umebaini kuwa uhalifu wa kivita ni wa kiwango cha kutisha katika Taifa hilo.
Kwa mujibu wa uchunguzi huo, wahanga wakubwa wa machafuko hayo ni wanawake na wasichana.
Makamu Mwendesha Mashitaka wa ICC, Nazhat Shameem Khan, alisema hakuna neno sahihi la kutumia katika kueleza unyanyasaji dhidi ya kundi hilo unaoendelea Darfur.
Ikumbukwe, Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa ndilo lililoiruhusu ICC kuendesha uchunguzi juu ya hali ilivyo nchini Sudan.
Published:


