18.4 C
New York

Ndidi kuondoka Uturuki, kutua Saudia

Published:

ISTANBUL, Uturuki

NAHODHA wa timu ya soka ya Taifa ya Nigeria (Super Eagles), Wilfred Ndidi, ataondoka Besiktas ya Uturuki na kujiunga na moja ya klabu za Ligi Kuu ya Saudi Arabia.

Ndidi ana msimu mmoja tu Besiktas aliyojiunga nayo mwaka 2025 kwa euro milioni 8 akitokea Leicester City.

Kwa mujibu wa ripoti zilizopo Uturuki, nyota huyo wa eneo la kiungo atatimkia Saudia majira haya ya kiangazi.

Taarifa za kuondoka kwake zinakuja wakati huu Ndidi akiwa amebakiza miaka miwili katika mkataba wake na Besiktas.

Besiktas imemteua kocha raia wa Italia, Vincenzo Italiano, baada ya kumfungashia virago Sergen Yalcin.

Related articles

Recent articles