TORONTO, Canada
MKONGWE wa timu ya soka ya Taifa ya Brazil, Ronaldo Nazario, amekosoa mbinu za kocha Carlo Ancelotti baada ya sare yao ya bao 1-1 dhidi ya Morocco.
Ronaldo (49), anaona haikuwa sahihi kwa uamuzi wa kocha huyo kumchezesha winga ya kushoto staa wa timu hiyo, Raphinha.
Raphinha, licha ya kucheza kushoto katika mechi nyingi akiwa Barcelona, amekuwa na kiwango bora zaidi anapotokea kulia.
Kwa mujibu wa Ronaldo, Ancelotti alifanya kosa la kiufundi kumtumia kama winga ya kushoto, hivyo kuinyima ushindi Brazil mbele ya Morocco.
“Raphinha kushoto, wakati amekuwa bora mno akicheza kulia pale Barcelona?,” alihoji Ronaldo aliyewahi kucheza Barcelona na Real Madrid.


