18.4 C
New York

Tunisia ya Herve Renard kuishangaza dunia?

Published:

MEXICO CITY, Mexico

BAADA ya kumtimua Sabri Lamouchi, timu ya soka ya Taifa ya Tunisia iko chini ya kocha maarufu raia wa Ufaransa, Herve Renard.

Lamouchi alifutwa kazi baada ya Tunisia kuchapwa mabao 5-1 na Sweden katika mechi yao ya kwanza msimu huu wa fainali za Kombe la Dunia.

Kocha huyo amekuwa na ‘damu mbaya’ na Watunisia kwa muda mrefu baada ya uamuzi wake wa kuikataa timu yao ya Taifa na kuchagua kuitumikia Ufaransa akiwa mchezaji.

Kwa upande mwingine, Lamouchi anakosolewa kwa kumuweka mmoja ya watoto wake kwenye benchi la ufundi la timu ya Taifa.

Wakati huo huo, kocha huyo amewakosoa mabosi wa Shirikisho la Soka la Tunisia kwa kumuingilia katika masuala ya kiufundi, ikiwamo kumpangia kikosi.

Je, Renard, kocha mwenye umri wa miaka 57 aliyewahi kuzinoa timu za taifa za Zambia, Ivory Coast na Saudi Arabia atabadili upepo katika kikosi cha Tunisia?

Ni kocha mzoefu aliyewahi kutwaa mara mbili taji la fainali za Mataifa ya Afrika (AFCON) akiwa na Zambia ‘Chipolopolo’ na Ivory Coast.

Katika fainali za Kombe la Dunia za mwaka 2022 zilizofanyika nchini Qatar, Renard aliiongoza Saudi Arabia kupata ushindi uliowashangaza wengi mbele ya Argentina ya Lionel Messi.

Amekabidhiwa benchi la ufundi la Tunisia ikiwa imebakiza mechi; dhidi ya Japan (Juni 21, 2026) na Uholanzi (Juni 25, 2026).

Related articles

Recent articles