22 C
New York

Mama amtoa machozi kipa wa Cape Verde

Published:

NEW YORK, Marekani

MLINDA mlango wa timu ya soka ya Cape Verde, Vozinha, amesema kutokuwepo uwanjani kwa mama yake ndiyo sababu ya kilio chake baada ya mechi yao dhidi ya Hispania.

Vozinha (40), alifanya kazi kubwa ya kuokoa mabao saba ya wazi na kuiwezesha Vape Verde kuambulia pointi moja katika mchezo huo wa Kombe la Dunia.

Ameandika historia ya kuwa kipa mwenye umri mkubwa zaidi kutokuruhusu bao katika mechi ya kwanza ya Kombe la Dunia.

“Nililia kwa sababu nililelewa na bibi na babu yangu, na mbaya zaidi hawapo leo hii nikiwa na mafanikio. Walifariki miaka michache iliyopita.

“Mama yangu naye amekosekana uwanjani kutokana na kukosa viza na gharama zingine. Tulichelewa kujipanga,” amesema.

Related articles

Recent articles