13.9 C
New York

Mambo 10 kuhusu Zubimendi wa Arsenal

Published:

LONDON, England
ARSENAL wamekamilisha usajili wa kiungo wa kimataifa wa Hispania, Martin Zubimendi, aliyetua klabuni hapo akitokea Real Sociedad kwa ada ya Pauni milioni 60.
Makala haya yanakuibulia mambo 10 kuhusu staa huyo aliyesaini mkataba wa miaka mitano pale Emirates.

  • Zubimendi (26), anakuwa mchezaji wa pili kutua Arsenal majira haya ya kiangazi baada ya kipa kutoka Chelsea, Kepa Arrizabalaga.
  • Zubimendi aliyeibuliwa na ‘academy’ ya Sociedad, aliikataa Liverpool iliyotaka kumsajili mwaka jana.
  • Kiungo wa ulinzi huyo mwenye umri wa miaka 26, amecheza mechi 236 akiwa na Sociedad, akifunga mabao 10.
  • Alikuwa sehemu ya kikosi cha Hispania kilichotwaa taji la Euro 2024, akitokea benchi kuchukua nafasi ya Rodri.
  • Ameshacheza mechi 19 akiwa na kikosi cha Hispania, ikiwamo fainali ya Nations League dhidi ya Ureno, ambayo alifunga bao, kabla ya kupoteza kwa penalti.
  • Ujio wa Zubimendi umelenga kuiimarisha safu ya kiungo ya Arsenal baada ya Thomas Partey na Jorginho kufungasha virago.
  • Katika moja ya mahojiano yake, amewahi kusema alikuwa akipenda kumtazama Xabi Alonso tangu akiwa mdogo.
  • Alonso, ambaye kwa sasa anainoa Real Madrid, ni miongoni mwa makocha ‘waliompika’ akiwa timu ya vijana ya Sociedad.
  • Msimu uliopita wa La Liga, Zubimendi aliingia ‘top 5’ ya viungo wenye pasi nyingi zilizofikia walengwa.
  • Akizungumzia kujiunga na Arsenal, Zubimendi alisema: “Nimeipenda Arsenal kutokana na aina ya uchezaji wao, inaendana na mimi.”
  • Kocha wa Arsenal, Mikel Arteta, alimzungumzia akisema: “Martin ni mchezaji ambaye si ataongeza ubora na ubunifu kwenye timu yetu.”

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img