15.5 C
New York

Polisi wavamia mazishi ya Jota

Published:

MERSEYSIDE, England
POLISI wamelazimika kuingilia kati na kuzuia kundi la mashabiki waliokuwa wakipiga picha katika kaburi la staa wa Liverpool na timu ya taifa ya Ureno, Diogo Jota.
Jota aliyefariki kwa ajali ya gari hivi karibuni, alizikwa leo nchini Ureno, ‘akipumzishwa’ kando na kaburi la kaka yake, Andre Silva, ambaye pia alikuwamo kwenye ajali hiyo.
Wawili hao wamezikwa mjini Igreja Matriz de Gondomar, eneo lililoko karibu na Mji wa Porto.
Taarifa zinaeleza kuwa baada ya mazishi, ambayo yalihudhuriwa pia na mastaa wa Liverpool, mashabiki walirudi na kuanza kupiga ‘selfie’ katika kaburi la mchezaji huyo.
Baada ya kupata taarifa, polisi walifika na kufanikiwa kuwaondosha mashabiki hao.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img