15.5 C
New York

Guardiola kuchukua kipa Barca

Published:

MANCHESTER, England
KOCHA wa Manchester City, Pep Guardiola, amewataka mabosi wake kuhakikisha wanainasa saini ya mlinda mlango wa Barcelona, Marc-Andre ter Stegen.
Man City, baada ya kukosa mataji yote msimu uliopita, imeshatumia Pauni milioni 100 kwenye usajili wa majira haya ya kiangazi.
Ikumbukwe, kiasi hicho cha fedha kimetumika kuzinasa saini za Rayan Ait-Nouri, Tijjani Reijnders, Rayan Cherki na Marcus Bettinelli.
Kwa upande wa ter Stegen, kocha Guardiola anaamini Mjerumani huyo anatosha kuziba pengo la Ederson anayehusishwa na mlango wa kutokea pale Etihad.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img