15.5 C
New York

Sterling kutimkia Saudia?

Published:

LONDON, England
KLABU za Ligi Kuu ya Saudi Arabia zinapigana vikumbo kuiwania saini ya winga wa Chelsea, Raheem Sterling.
Sterling aliyecheza kwa mkopo Arsenal, ameshaambiwa wazi na uongozi wa Chelsea kuwa hayuko kwenye mipango yake ya msimu ujao.
Chelsea wamefikia hatua hiyo baada ya kukamilisha usajili wa winga Jamie Gittens.
Mbali ya Al Nassr, vigogo wenzao wa Saudia, Al Hilal, nao wameripotiwa kuimezea mate huduma ya nyota huyo mwenye umri wa miaka 30.
Katika hatua nyingine, wakali wa soka la Uturuki, Besiktas, nao wameripotiwa kuiwinda saini ya Sterling.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img