14.7 C
New York

Ramos: Nileteeni Madrid robo fainali

Published:

MEXICO CITY, Mexico

NAHODHA wa zamani wa Real Madrid, Sergio Ramos, amesema ni ndoto yake kukutana na timu hiyo katika hatua ya robo fainali ya Kombe la Dunia kwa ngazi ya Klabu.

Ramos kwa sasa ni mchezaji wa Monterrey ya Mexico, ambayo itaingia robo fainali endapo itaing’oa Borussia Dortmund katika hatua ya 16 bora, mchezo utakaochezwa keshokutwa.

Madrid wao watawakabili wakali wa Ligi Kuu ya Italia (Serie A), Juventus, katika mchezo mwingine wa 16 bora utakaochezwa kesho.

Hivyo, endapo Madrid wataing’oa Juventus, kisha Monterrey wakaifunga Dortmund, basi ndoto ya Ramos kuvaana na mabosi wake wa zamani itakuwa imetimia.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img