14.7 C
New York

Nabi yajayo yanafurahisha ‘Sauzi’

Published:

JOHANNESBURG, Afrika Kusini
BEKI wa zamani wa Kaizer Chiefs, Mokete Tsotetsi, anaamini timu hiyo inayonolewa na kocha Nasreddine Nabi itakuja kivingine msimu ujao.

Kaizer ilimaliza msimu uliopita ikiwa nje ya nafasi nane za juu kwenye msimamo wa Ligi Kuu ya Afrika Kusini (PSL).

Hata hivyo, ukiwa ni msimu wa kwanza chini ya Nabi aliyewahi kuinoa Yanga, Kaizer ilimaliza ukame wa mataji baada ya kujinyakulia Kombe la Ligi (Nedbank Cup).

Kuelekea msimu ujao, Kaizer wataweka kambi nchini Uholanzi, jambo ambalo mkongwe wao, Tsotetsi, amelizungumzia akisema:

“Kwenda Uholanzi ni vizuri … Uholanzi ni wazuri kiufundi, hivyo nafikiri itaisaidia Chiefs kuandaa kikosi imara. Nafikiri watarudi wakiwa tofauti na bora Zaidi.”

Katika kujiweka sawa kwa ajili ya msimu ujao, kocha Nabi amekifanyia marekebisho makubwa kikosi chake, ikiwamo kuwafungulia mlango wa kutokea nyota wake watano.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img