14.7 C
New York

Nyuma ya pazia mkataba wa Ronaldo

Published:

RIYADH, Saudi Arabia
BAADA ya kusaini mkataba mpya wa miaka miwili, sasa staa wa Al-Nassr, Cristiano Ronaldo, atavuna Pauni milioni 492 (zaidi ya Sh tril. 1.7 za Tanzania).

Huo ni mshahara tu, hivyo ‘CR7’ anaingia kwenye historia ya kuwa na mkataba ghali zaidi katika ulimwengu wa michezo.

Iko hivi; fedha hizo ni sawa na kusema Ronaldo mwenye umri wa miaka 40 atakuwa akilipwa Pauni 488,000 (Sh bil. 1.7 za Tanzania) kwa siku.

Aidha, kusaini mkataba kumekwenda sambamba na makubaliano kwamba sasa Ronaldo atamiliki asilimia 15 ya hisa za klabu ya Al-Nassr.

Nje ya hapo, Ronaldo anatarajiwa kutangazwa kuwa balozi wa soka la Saudi Arabia, dili ambalo litampa si chini ya Pauni milioni 60 (Sh bil. 216 za Tanzania).

Ndani ya uwanja, licha ya umri kusogea, bado Ronaldo ameweza kufunga mabao 99 katika mechi 111 alizocheza tangu aliposajiliwa na klabu hiyo mwaka 2022.

Msimu uliopita, aliingia kambani mara 35 katika mechi 41 na kuibuka mfungaji bora wa Ligi Kuu hiyo ya Saudia kwa mara ya pili mfululizo.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img