14.7 C
New York

Kessie akili yote Serie A

Published:

MILAN, Italia
RIPOTI zinaeleza kuwa kiungo wa zamani wa AC Milan, Franck Kessie, ameanza kutamani kurudi Ligi Kuu ya Italia (Serie A).

Kessie mwenye umri wa miaka 28, alitua Al-Ahli ya Saudi Arabia mwaka juzi akitokea La Liga alikokuwa akiitumikia Barcelona.

Sasa, taarifa zinaeleza kuwa nyota huyo wa kimataifa wa Ivory Coast anaitamani AS Roma kwa kuwa inanolewa na kocha wake wa zamani, Gian Piero Gasperini.

Hata hivyo, changamoto kubwa inayoweza kuizuia Roma kumsajili ni dau kubwa la euro milioni 14 wanalotaka Al-Ahli.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img