14.7 C
New York

Mbappe fiti kuivaa Juve

Published:

MADRID, Hispania
UWEZEKANO ni mkubwa kwa mshambuliaji wa Real Madrid, Kylian Mbappe, kuikabili Juventus katika mchezo wa keshokutwa.
Madrid itavaana na vigogo hao wa Serie A, ukiwa ni mtanange wa hatua ya 16 bora ya Kombe la Dunia kwa ngazi ya Klabu.
Ikumbukwe, Mbappe hajacheza hata mechi moja ya michuano hiyo kutokana na maumivu ya tumbo aliyoyapata kabla ya mechi yao ya kwanza.

Sasa, kwa mujibu wa taarifa, Mfaransa huyo alijumuhika kwenye mazoezi ya kabla ya mchezo uliopita dhidi ya RB Salzburg lakini kocha Xabi Alonso aliamua kumpa muda wa kuendelea kujiweka fiti.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img