22.6 C
New York

Kubeti  kwachangia bilioni 17 pato la Taifa

Published:

Na Mwandishi Wetu

Waziri wa Fedha Dk. Mwigulu Nchemba amesema hadi kufikia Aprili, 2025, Bodi ya

Michezo ya Kubahatisha Tanzania imekusanya jumla ya Sh 17.42 bilioni  sawa na asilimia 70 ya lengo la mwaka .

Akiwasilisha hotuba ya Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Fedha kwa mwaka wa Fedha 2025/2026 Bungeni Jijini Dodoma leo June 04,2025, Mwigulu amesema; 

Amesema mwaka 2024/25, Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania ilipanga kukusanya mapato yatokanayo na michezo ya kubahatisha ya jumla ya Sh24.89 bilioni .

“Kwa mwaka 2025/26, Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania imepanga: Kutoa leseni 14,124 ikijumuisha leseni mpya 845 na kuhuisha leseni 13,279; kufanya kaguzi 12 kwa kuzingatia vihatarishi; kutekeleza operesheni  za kudhibiti michezo haramu; kukusanya mapato ya jumla ya shilingi bilioni 29.89,” amesema Waziri Nchemba.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img