20.1 C
New York

Bunge lapitisha  Sh 2.746 Trilioni  bajeti ya Wizara ya Uchukuzi

Published:

Na Mwandishi Wetu

Bunge la Tanzania limeidhinisha Bajeti ya Wizara ya Uchukuzi yenye jumla ya Sh 2.746 trilioni kwa ajili ya utekelezaji wa majukumu yake kwa mwaka wa fedha 2025/2026.

Kati ya fedha hizo, Sh 125.4 bilioni zimetengwa kwa  matumizi ya kawaida huku sh 2.621  trilioni  zikitengwa kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo.

Akiwasilisha hotuba ya makadirio ya mapato na matumizi ya Wizara hiyo Bungeni, Waziri wa Uchukuzi, Prof. Makame Mbarawa ameeleza kuwa kati ya fedha za matumizi ya kawaida, sh 96.7 bilioni  ni kwa ajili ya mishahara ya watumishi na Sh 28.8 bilioni ni kwa matumizi mengineyo.

Aidha, kati ya fedha za miradi ya maendeleo, Sh 2.45 trilioni ni fedha za ndani na Sh 168.5 bilioni  ni fedha za nje.

Amesema katika utekelezaji wa bajeti hiyo, wizara itaendelea na miradi ya kielelezo kama ujenzi wa Reli ya Kisasa ya (SGR) na uboreshaji wa Kampuni ya Ndege Tanzania (ATCL), sambamba na miradi ya kimkakati kama uboreshaji wa Bandari ya Dar es Salaam, ujenzi wa viwanja vya ndege mbalimbali nchini na uboreshaji wa usalama katika usafiri kwa njia ya maji na anga.

“Serikali pia itaendelea na ujenzi wa meli nne za mizigo kwa ubia na sekta binafsi ili kuimarisha biashara kati ya Tanzania na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), kupitia Bandari ya Kigoma na Bandari ya Dar es Salaam ambapo ujenzi wa meli hizo unatarajiwa kukamilika ndani ya miaka miwili.

Ameeleza kuwa katika kuboresha huduma na miundombinu ya usafiri wa anga, ardhi na maji, Serikali itatekeleza miradi kama vile ujenzi wa Chuo cha Usafiri wa Anga, uimarishaji wa reli za MGR na TAZARA, pamoja na kuanzisha Kampasi ya NIT Lindi itakayotoa mafunzo katika sekta ya usafiri kwa njia ya maji, mafuta na gesi.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img