12.9 C
New York

Waandishi waendelea kumkaanga Trump

Published:

WASHINGTON DC, Marekani

WAANDISHI wa habari wa CNN na MS NOW wamedai kuzuiwa kuingia kwenye hafla ya chakula cha usiku iliyofanyika Ikulu ya Marekani, wakisisitiza kuwa huko ni kukiuka agizo la Mahakama.

Awali, vyombo hivyo, pamoja na Politico, vilizuiwa kutekeleza majukumu yake ndani ya Ikulu kwa kile Rais Donald Trump alichodai kuwa vimekuwa vikieneza taarifa za uongo.

Vyombo hivyo vilifika mahakamani kufikisha malalamiko yao, kabla ya muhimili huo wa kutafsiri sheria kumtaka Rais Trump kuondosha zuio hilo.

Katika agizo lake, Mahakama ilieleza kuwa kuwazuia waandishi ni kinyume cha Katiba, hivyo Ikulu inapaswa kuachana na hatua hiyo mara moja.

Hata hivyo, waandishi wa CNN na MS NOW wameibuka tena na kusema Ikulu ya Marekani imepuuza agizo la Mahakama kwa kuwazuia kuingia kwenye hafla ya jana Septemba 24, 2026.

Related articles

Recent articles