14.8 C
New York

Papa Leo kuanza ziara yake Ufaransa

Published:

PARIS, Ufaransa

KIONGOZI wa Kanisa Katoliki duniani, Papa Leo XIV, anaanza ziara yake ya siku nne mjini Paris, Ufaransa, huku waumini takribani 600,000 wakitarajiwa kumpokea.

Rais wa Ufaransa, Emmanuel Macron, alitarajiwa kumpokea Papa katika Uwanja wa Ndege asubuhi ya leo Septemba 25, 2026.

Baada ya kumpokea, wawili hao wangejadili masuala kadhaa, ikiwamo teknolojia ya akili-unde [AI]. Rais Macron atahutubia pia akiwa na Papa mjini Metz.

Hata hivyo, taarifa zinaeleza kuwa Rais huyo hatohudhuria ibada zitakazoongozwa na Papa ikiwa ni katika kuheshimu sheria inayoitaka Serikali kujitenga na masuala ya dini.

Na badala yake, atakayehudhuria ni mkewe, Brigitte, Waziri Mkuu wa nchi hiyo, Sebastien Lecornu, pamoja na wanasiasa wengine, wakiwamo wanaowania urais katika Uchaguzi Mkuu ujao [2027].

Ziara ya Papa nchini Ufaransa inakuja wakati zikiwapo taarifa zinazodai kuwa Rais Macron hana mahusiano mazuri na mamlaka za Vatican.

Related articles

Recent articles