MILAN, Italia
SERIKALI ya Italia imepitisha sheria inayopiga marufuku wanafuzi wa kike kuvaa niqab [vazi linaloficha uso] wawapo shuleni.
Hata hivyo, sheria hiyo imeweka wazi kuwa katazo hilo halihusiani na hijab kwani vazi hilo halifichi uso wa mvaaji.
Wakati huo huo, hatua hiyo imeenda sambamba na katazo la wanafunzi wengi wasiozungumza Kiitalia kuwekwa darasa moja.
Mabadiliko hayo yameungwa mkono na Waziri Mkuu, Giorgia Meloni, akisema hayalengi kuigawa bali kuiunganisha jamii na urithi wa nchi hiyo.
Kuhusu ishu ya wanafunzi kuzuiwa kuvaa niqab, Waziri wa Elimu, Giuseppe Valditara, amesema lengo ni kuimarisha usawa wa kijinsia. “Unapaswa kwenda shule ukiwa haujafunika uso wako.


