12.9 C
New York

Chelsea yamtaka kinda wa Gambia

Published:

LONDON, Uingereza

CHELSEA ni moja ya klabu zilizoingia vitani kuisaka saini ya kiungo wa U-17 ya Gambia, Adama Jeng.

Jeng mwenye urefu wa futi 6 na inchi 2, ana umri wa miaka 15 na ni miongoni mwa nyota wanaoibeba U-17 ya Gambia katika michuano ya WAFU Zone A iliyomalizika huko Senegal.

U-17 ya Gambia, maarufu pia kwa jina la ‘Baby Scorpions’, ilitwaa ubingwa kwa ushindi wa penalti 5-3.

Taarifa zinaeleza kuwa mbali na Chelsea, klabu zingine kubwa za Ulaya zinazomtolea macho chipukizi huyo ni Bayern Munich, Benfica, Sporting Lisbon na Paris FC.

Katika hatua nyingine, klabu zilizotajwa kuunga na hizo katika mBio za kumsajili kinda huyo ni Monaco na Union Saint-Gilloise.

Related articles

Recent articles