RIO, Brazil
MKONGWE wa soka la Brazil, Carlos, amefichua kuwa Cristiano Ronaldo ana miaka mingine 10 ya kuendelea kucheza soka kabla ya kustaafu.
Carlos akihojiwa na kituo cha televisheni cha AS amesema hamuoni Ronaldo akipoteza ubora wake kwa miaka ya hivi karibuni.
Kauli yake hiyo ilikuja kabla ya Ureno ya Ronaldo kuivaa Wales jana Septemba 24, 2026, na kuibuka na ushindi wa bao 1-0, mfungaji akiwa ni Joao Felix.
“Anaweza kucheza tena kwa miaka mingine 10,” amesema Carlos na kuongeza kuwa Ronaldo ni miongoni mwa wachezaji bora wachache aliowahi kuwaona kwenye ulimwengu wa soka.
“Bado yuko fiti kimwili, anafurahia pia kuitumikia timu yake ya Taifa ya Ureno na anatamani kuendelea kucheza soka,” amesema Carlos.


