LONDON, Uingereza
LICHA ya kusajiliwa kwa matumaini makubwa ya kuingia kikosi cha kwanza, mambo yamekuwa tofauti kwa Alejandro Garnacho tangu atue Aston Villa.
Kwa sasa, zipo taarifa zinazodai kuwa anaweza kujiunga na moja ya klabu za Ligi Kuu ya Hispania [La Liga].
Mshambuliaji huyo raia wa Argentina alijiunga na Villa akitokea Chelsea kwa mkopo wa msimu mmoja.
Tangu ajiunge na Villa, nyota huyo hajaweza kuingia kikosi cha kwanza cha kocha Unai Emery na badala yake amecheza dakika 31 pekee.
Katika mechi mbili zilizopita, Garnacho alimaliza zote akiwa benchi na huenda asingecheza kabisa mchezo dhidi ya Tottenham kama si Alysson kupata majeraha.


