12.9 C
New York

Netanyahu: Israel haikosei kushambulia Iran, Gaza

Published:

JERUSALEM, Israel

WAZIRI Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu, haoni kama Serikali yake ilifanya kosa kutekeleza mashambulizi ya kijeshi Iran, Gaza na maeneo mengine ya Mashariki ya Kati.

Katika hotuba yake kwenye Mkutano wa Umoja wa Mataifa, Netanyahu amesema Israel itaendelea kushambulia kila inayemuona kuwa ni adui wake au kibaraka wa ugaidi. “Tutaendelea. Hakuna namna,” amesema.

Aidha, Netanyahu amesisitiza kuwa hakubaliani na shutuma zinazodai kuwa Israel inahusika katika mauaji ya halaiki katika Ukanda wa Gaza.

Ujumbe wake huo unatafsiriwa kuwa ni majibu kwa hotuba aliyokuwa ameitoa Rais wa Palestina, Mahmoud Abbas, katika Mkutano huo.

Abbas alisema Israel inatekeleza mauaji ya kinyama dhidi ya watu wasio na hatia katika Ukanda huo wa Gaza. “Wapalestina wanauawa, makazi yao yanaharibiwa na kulazimishwa kuhama …” alisema Abbas.

Related articles

Recent articles