MERSEYSIDE, Uingereza
HATIMAYE mshambuliaji raia wa Ufaransa, Bradley Barcola, amejiunga na Liverpool akitokea PSG, usajili huo ukigharimu kitita cha Pauni milioni 123.
PSG walitaka Pauni milioni 145 kumwachia nyota huyo mwenye umri wa miaka 23, lakini Liverpool imetanguliza Pauni milioni 106, kisha itaongezeka Pauni milioni 17.
Barcola amesaini mkataba wa miaka mitano na Liverpool na anakuwa mchezaji wa tano kusajiliwa na klabu hiyo majira haya ya kiangazi.
Itakumbukwa kuwa tayari ‘Majogoo’ hao wa Anfield wamezinasa saini za winga Victor Munoz na mabeki Jeremy Jacquet, Ronald Araujo na Ifeanyi Ndukwe.
Barcola, ambaye atavaa jezi namba 29 na anavutiwa zaidi kucheza winga ya kushoto na ujio wake ni baada ya Liverpool kumpoteza Mohamed Salah.
Msimu uliopita, nyota huyo aliifungia Liverpool mabao 13 na kutoa asisti saba katika mechi 49 za mashindano yote waliyoshiriki PSG.


