22.5 C
New York

Watkins: Sikutaka kuondoka Villa

Published:

LONDON, Uingereza

STRAIKA Ollie Watkins ameeleza masikitiko yake ya kuondoka klabuni hapo, akisema hakupenda kuachana nayo kwa staili hiyo.

Watkins (30), amejiunga na Al-Hilal ya Ligi Kuu ya Saudi Arabia kwa mkataba wa miaka mitatu baada ya Villa kupokea kitita cha Pauni milioni 51.

Kuondoka kwake Villa ni baada ya kuitumikia klabu hiyo ya England kwa miaka sita, akifunga mabao 108 na asisti 47.

Kwa upande mwingine, Watkins ndiye mfungaji bora wa Villa katika historia ya Ligi Kuu ya England akiwa amezifumania nyavu mara 91.

Msimu uliopita, mshambuliaji huyo aliifungia Villa jumla ya mabao 16 katika mechi 37 za Ligi Kuu hiyo.

Related articles

Recent articles