23.5 C
New York

Aziz Ki, Mobetto kama mastaa hawa tu

Published:

Na Hassan Mwasha, Gazetini

MOJA ya ‘kapo’ zenye nguvu na ushawishi mkubwa mitandaoni ni hii ya kiungo wa Yanga raia wa Burkina Faso, Stephanie Aziz Ki, na mrembo wa Tanzania, Hamisa Mobetto. Kutoka uchumba na sasa ni wawili hao ni mke na mume.

Wawili hao walikutana wakiwa tayari ni mastaa. Usta awa Aziz Ki ulitokana na mchezo wa soka, wakati Mobetto alianza kupata jina akiwa mwigizaji wa muvi za Bongo, ingawa baadaye alijitosa katika uanamitindo.

Kwa upande mwingine, Aziz Ki na Mobetto siyo kapo pekee au ya kwanza inayohusisha mwanasoka na mwigizaji. Kwa taarifa yako tu, orodha ni ndefu mno.

Unamkumbuka kiungo wa zamani wa timu ya soka ya Taifa ya Uholanzi, Wesley Sneijder? Kama ilivyo kwa Aziz Ki, Sneijder aliyewahi pia kuzitumikia Inter Milan na Galatasaray naye alioa mwigizaji.

Ndiyo, mwanasoka huyo alifunga ndoa na mlimwende aitwaye Yolanthe Cabau, ambaye ni maarufu mno katika tasnia ya filamu na tamthilia nchini kwao, yaani Uholanzi.

Yolanthe alianza kuigiza tangu akiwa na umri wa miaka 17 lakini ‘alitoboa’ na kuipata jina kubwa baada ya kazi nzuri aliyoifanya kwenye tamthilia maarufu ya ONM.

Achilia mbali hao, kuna kapo nyingine ya Francesco Totti na Ilary Blasi. Totti, kama ilivyo kwa Aziz Ki na Sneijder, naye alifunga ndoa na staa wa tasnia ya maigizizo.

Totti, mshambuliaji wa zamani wa timu ya soka ya Taifa ya Italia, alimuoa Ilary, ambaye alikutana naye alipokuwa akiitumikia klabu kongwe ya Serie A, AS Roma. Mrembo huyo ni mwigizaji, mwanamtindo mwenye jina kubwa katika ardhi ya Italia.

Related articles

Recent articles