NEW YORK, Marekani
STAA wa tenesi raia wa Serbia, Novak Djokovic, ameishia raundi ya kwanza ya michuano ya US Open.
Safari yake kwenye michuano hiyo imeishia mikononi mwa Mariano Navone aliyemfunga katika seti zote tano.
Kwa kufungwa na Navone, Djokovic amekosa fursa ya kufikisha mataji makubwa 25 katika maisha yake ya tenesi.
Katika mechi yake dhidi ya Djokovic, Navone anayeshika nafasi ya 49 kwenye viwango vya dunia alishinda kwa seti 7-6 (7-5), 5-7, 4-6, 6-2, 6-1.
Mechi hiyo ilimalizika ikiwa imedumu kwa saa 4 na dakika 36. Hii inakuwa mechi iliyochezwa muda mrefu zaidi katika ufunguzi wa msimu wa US Open.


