Na Hassan Mwasha, Gazetini
HATUA ya Dk. Emmanuel Nchimbi kujiuzulu nafasi ya Makamu wa Rais, na kisha kuvulishwa uanachama wa Chama cha Mapinduzi (CCM) imemuibua mchambuzi wa siasa na Mhadhiri wa Siasa na Uchumi kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Dk. Richard Mbunda, akisema siasa za sasa zimejaa ‘uchawa’, fitina na chuki.
Dk. Nchimbi alitangaza kupitia mitandao ya kijamii Agosti 25, 2026, kwamba amemwandikia barua ya kujiuzulu ‘bosi’ wake, Rais Dk. Samia Suluhu Hassan, kabla ya Kikao cha Halimashauri Kuu ya Taifa kukaa jana Agosti 26, 2026 na kutangaza kumng’oa ndani ya Chama.
KWANINI SASA?
GAZETINI lilimtafuta Dk. Mbunda ili kupata maoni yake juu ya matukio yote mawili ya Dk. Nchimbi; kujiuzulu nafasi ya Makamu wa Rais na kuvuliwa uachama ndani ya CCM aliyoitumikia kwa miaka mingi.
Kwa upande wake, Dk. Mbunda alisema kwa pamoja matukio hayo yamebeba uzito mkubwa, ikizingatiwa kuwa yanatokea katika kipindi ambacho Tanzania inapitia kile alichokiita ‘mkwamo wa kisiasa’.
Akieleza zaidi, Dk. Mbunda alisema kwa kipindi hiki, ambacho Tanzania inapitia ukosolewaji mkubwa kutoka ndani na nje ya nchi baada ya kile kilichotokea Oktoba 29, 2026, Serikali ilipaswa kuwa kitu kimoja na si hiki kinachotokea.
“Ukiniuliza mimi, nitakwambia Dk. Nchimbi alikuwa anafanya kazi kubwa katika kuipatanisha Serikali na jamii,” alisisitiza Dk. Mbunda.
UCHAWA, FITINA CHANZO?
Kwa upande mwingine, GAZETINI lilipotaka kufahamu kama Dk. Mbunda anaiona changamoto iliyosababisha Dk. Nchimbi kung’atuka katika kiti cha Makamu wa Rais alichokalia kwa kipindi kufupi kisichotimia mwaka mmoja.
Akijibu hilo, Dk. Mbunda alisema si rahisi kufahamu kwa undani kile kilichosukuma uamuzi wake huo, ila anaona siasa za sasa zikiwa zimejaa ‘uchawa’ na fitina, hivyo kuathiri ufanisi wa kiutendaji.
“Kwa sasa, kumejaa uchawa, fitina na majungu. Kila anayefika kwa kiongozi, anajitahidi kufitinisha wenzake ili waonekana wabaya,” amesema Dk. Mbunda.
DK. NCHIMBI KUIBUKIA HUKU?
Katika barua ya kujiuzulu aliyoisambaza mitandaoni, Dk. Nchimbi aliweka wazi kuwa anastaafu siasa moja moja, lakini hisia za wengi ni kwamba hatua ya kufutiwa uanachama wa CCM inaweza kusababisha uamuzi wa hasira na kujiunga na upinzani.
GAZETINI ilipotaka kupata mtazamo wake juu ya hilo, Dk. Mbunda alisema: “Wanasisasa hawatabiriki. (Dk. Nchimbi) aliwahi kusema anastaafu siasa mwaka 2015 lakini alirudi, akapanda ngazi hadi kuwa Makamu wa Rais.
“Kuhusu kwenda upinzani, nafikiri kama angetaka angejiunga nao mwaka 2015 baada ya (Edward) Lowassa kwenda huko. Alikuwa kijana wa Lowassa. Aliamua kubaki CCM. Hivyo, sioni akibadilika.”
HISTORIA INAKUMBUSHA
Dk. Nchimbi anaingia kwenye historia ya viongozi wa ngazi za juu wa Serikali waliowahi kuachia ngazi. Mwalimu Julius Nyerere aliwahi kujiuzulu akiwa ‘Waziri Mkuu wa Tanganyika’ mwaka 1962 na kumwachia kijiti Rashid Mfaume Kawawa.
Mwaka 1977, Ali Hassan Mwinyi akiwa Waziri wa Mambo ya Ndani alilazimika kujiweka kando pia, sababu ikiwa ni mauaji ya vikongwe katika mikoa ya Mwanza na Shinyanga.
Mwaka 1984, Abdul Jumbe akiwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Rais wa Zanzibar, alijiuzulu nyadhifa zake zote kwa kile alichokiita ‘uchafuzi wa hali ya hewa ya kisiasa’.
Pia, mwaka 1990, mawaziri wote wa Tanzania, akiwamo Waziri Mkuu, Sinde Warioba, walijiuzulu kwa sababu ya kashfa ya rushwa na malalamiko ya wananchi, wakati huo Rais akiwa Mzee Mwinyi.
Mwaka 2015, Edward Lowasa naye alijiuzulu nafasi ya Waziri Mkuu kutokana na kashfa ya kodi ya kampuni ya kufua umeme ya Richmond. Mwaka huo pia, Sospeter Muhongo akiwa Waziri wa Nishati na Madini naye alijiuzulu kutokana na skendo ya Tegeta Escrow.
Mwaka 2025, Humphrey Polepole akiwa Balozi wa Tanzania nchini Cuba, alitangaza kujiuzulu kwa kile alichoeleza kutoridhishwa na mienendo na taratibu za chama tawala (CCM).


