22.2 C
New York

China inavyoua biashara ya magari Ujerumani

Published:

BERLIN, Ujerumani

BMW imekuwa kampuni ya tano ya utengenezaji magari nchini Ujerumani kutangaza kupunguza wafanyakazi. Kampuni zilizotangulia kuchukua hatua hiyo ni VW, Porsche na Mercedes-Benz.

Hatua ya kupunguza ajira inaelezwa kuchangia kuporomoka kwa biashara ya magari ya kampuni hizo za Ujerumani, hiyo ikitokana na ushindani mkali kutoka China.

Kampuni ya BMW yenye makao makuu yake mjini Munich, ambayo ndiyo inayomiliki magari ya kifahari ya Rolls-Royce, itapunguza ajira takribani 8,000 duniani, saw ana asilimia 5 ya nguvu kazi yake.

Awali, BMW ndiyo iliyoonekana kutunishiana misuli na kampuni za magari za China lakini tangazo la kupunguza wafanyakazi linatoa picha tofauti.

Kwa mujibu wa waatalamu wa magari, BMW imeshindwa kwenda na kasi ya ubunifu na teknolojia ya magari ya umeme (EV) inayotumiwa na kampuni za China kwa sasa.

Mwaka 2025, uingizaji wa magari ya BMW nchini China ulishuka kwa kiasi kikubwa. Takwimu zinaeleza kuwa anguko ni asilimia 30 kwa mwaka.

Hivi karibuni, BMW iliweka wazi kuwa faida yake ya robo ya pili yam waka imeshuka kwa asilimia 35, huku mapato nayo yakiporomoka kutoka euro bilioni 34 hadi euro bilioni 31.

Ni hivi karibuni tu, kampuni nyingine ya Porsche ilitangaza mpango wake wa kupunguza ajira 5,000 ifikapo mwaka 2035. Kwamba mmoja kati ya wafanyakazi watano atapoteza ajira.

Mwaka 2025, Porsche inayotengeneza magari ya Volkswagen, ilitangaza mpango wake wa kupunguza wafanyakazi 1,900 mjini Stuttgart hadi kufikia 2029. Tayari imeshakata wafanyakazi 500 katika ofisi za mjini Leipzig.

Related articles

Recent articles