21.6 C
New York

Nchi zilizo hatarini kwa kufanya biashara na Iran

Published:

WASHINGTON DC, Marekani

HIVI karibuni, Marekani ilizitangazia ‘kiama’ nchi zinazofanya biashara na Iran, ikisema nazo zitakumbana na vikwazo vya kiuchumi. Iran imekuwa kwenye vikwazo vya Marekani tangu ilipofanya mapinduzi ya Kiislam mwaka 1979.

China ni miongoni mwa washirika wakubwa wa kibiashara wa Iran. Ni mnunuaji mkubwa zaidi wa bidhaa zinazotoka katika Taifa hilo la Mashariki ya Kati. Kwa mwaka 2025, ilinunua asilimia 26.9 ya bidhaa zote zilizosafirishwa na Iran nje ya nchi.

Takwimu hizo ni kwa mujibu wa Kituo cha Kimataifa cha Biashara (ITC) kinachofanya kazi chini ya Umoja wa Mataifa (UN) na Shirika la Biashara Duniani.

Uturuki, licha ya kwamba pia inashirikiana kwa karibu na Marekani na China, pia ni mshirika mwingine mkubwa wa Iran katika eneo la kibiashara.

Ni kama ilivyo kwa Pakistan, ambayo inashirikiana na Marekani, lakini pia inafanya biashara kwa kiasi kikubwa na majirani zake, Iran.

Hata hivyo, tofauti na Uturuki, Pakistan inaitegemea mno Marekani kama mnunuzi wa bidhaa zake. Hivyo, endapo itawekewa vikwazo, Pakistan itakuwa kwenye wakati mgumu kiuchumi.

Armenia nayo ni mshirika mkubwa wa kibiashara wa Iran, ingawa inauza bidhaa zake nyingi (asilimia 34.9 kwa mwaka 2025) kwa Urusi.

Related articles

Recent articles