22.2 C
New York

Nchi zinazoongoza kwa uzalishaji wa dhahabu duniani

Published:

Na mwandishi wetu, Gazetini

CHINA ndiyo nchi inayoongoza kwa uzalishaji wa madini ya dhahabu duniani. Uzalishaji wake umeongezeka kwa asilimia 9 kutoka tani 351 mwaka 2010 hadi tani 384 mwaka 2025.

Kwa mujibu wa ripoti ya Baraza la Madini ya Dhahabu Duniani, Urusi imepanda kutoka nafasi ya tano na sasa ni ya pili, ikiwa imeongeza uzalishaji wake kwa asilimia 70 (2010-2025).

Katika nafasi ya tatu, ni Australia, ambayo uzalishaji wake kwa mwaka 2010 hadi 2025 umeongezeka kwa asilimia 14 kutoka tani 257 hadi tani 293.

Canada inafuata ikiwa na tani 213, sawa na ongezeko la asilimia 109, ukilinganisha na tani 102 za mwaka 2010.

Aidha, uzalishaji wa dhahabu kwa Marekani umeshuka kutoka tani 231 hadi tani 157 na sasa imeporomoka kutoka nafasi ya tatu hadi ya saba.

Ni kama ilivyo Afrika Kusini, ambayo uzalishaji wake umeshuka takribani mbili kutoka tani 210 hadi tani 99.

Kwa Afrika, Ghana imeongeza kwa asilimia 99 uzalishaji wa madini kutoka tani 187 na sasa inashika nafasi ya sita duniani.

Related articles

Recent articles