LONDON, Uingereza
BEKI wa zamani wa Manchester United, Rio Ferdinand, amemtabiria kocha wa Arsenal, Mikel Arteta, kutwaa tena taji la Ligi Kuu ya England (EPL) msimu huu wa 2026-27.
Washika Bunduki wameianza kwa kishindo safari yao msimu huu baada ya kupata ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Coventry.
Rio anaamini Arteta ana nafasi kubwa ya kuingia kwenye orodha ya makocha waliowahi kutetea ubingwa wa Ligi Kuu hiyo.
Akizungumza kupitia chaneli yake ya mtandao wa YouTube, Rio alisema Mhispania na uzoefu mkubwa wa EPL, ikilinganishwa na makocha anaoshindana nao Kwa sasa.
“Uzoefu alionao Mikel Arteta na makocha wengine ni tofauti kabisa. Na Kwa sasa anajua namna ya kushinda mechi zake,” amesema Rio.


