ISLAMABAD, Pakistan
WAZIRI Mkuu wa zamani wa Pakistan, Imran Khan, amerejeshwa gerezani akitokea hospitali alikokuwa akifanyiwa matibabu.
Taarifa zinadai kuwa Khan amerudi jela mjini Islamabad asubuhi ya leo Agosti 21, 2026, baada ya madaktari kuthibitisha kuwa afya yake iko imara.
Kwa mujibu wa Waziri wa Habari wa Pakistan, Attaullah Tarar, Khan alikutana na madaktari bingwa, wakiwamo wa magonjwa ya moyo.
Hatua ya kupelekwa hospitali na kukutana na madaktari kwa saa 48 ilitokana na agizo la Mahakama Kuu ya Pakistan kutaka afikishwe kwenye matibabu.
Khan amekuwa jela kwa miaka takribani mitatu, tangu alipohukimiwa mwaka 2023 kwa mashitaka ya rushwa alipokuwa Waziri Mkuu.
Awali, familia ya mwanasiasa huyo, akiwamo dada yake, Azma, ailiibuka na kutoa madai kuwa imekuwa ikizuiwa kwenda kumuona gerezani.


