27.5 C
New York

Waasi waua wanajeshi Mali

Published:

BAMAKO, Mali

WANAJESHI zaidi ya 10 wameripotiwa kuuawa baada ya kambi yao kushambuliwa na kikundi cha waasi wikiendi iliyopita.

Jama’at Nusrat al-Islam wal-Muslimin (JNIM), ambalo ni kundi la kigaidi lenye ukaribu na al-Qaeda limethibitisha kuhusika katika shambulizi hilo.

Kwa mujibu wa shuhuda aliyehojiwa na kituo cha televisheni cha RFI, mapigano kati ya jeshi na waasi hao yalidumu kwa takribani saa mbili (dakika 120).

Taarifa zaidi zinaeleza kuwa wapiganaji wa JNIM walifanikiwa kuiteka kambi hiyo iliyoko katika Mji wa San.

Tukio hilo ni mwendelezo wa mengi yanayotoa picha ya usalama mdogo nchini Mali, hasa katika maeneo ya Kaskazini, ambako vikundi vya waasi wamekithiri.

Related articles

Recent articles