14.4 C
New York

MVP wa kwanza NBA afariki

Published:

LOS ANGELES, Marekani

MCHEZAJI wa kwanza katika historia ya Ligi Kuu ya Kikapu ya Marekani [NBA] kutwaa tuzo ya Mchezaji Bora wa Msimu [MVP], Bob Pettit, amefariki akiwa na umri wa miaka 93.

Pettit alitwaa tuzo hiyo mara mbili, ya kwanza akiibeba katika msimu wa 1955-56 na ya pili msimu wa 1958-59. Alimaliza misimu hiyo yote akiwa mfungaji bora.

Pia, historia ya NBA itakumbuka kuwa aliingia kwenye Kikosi Bora cha Msimu katika misimu yote 11 aliyocheza NBA. Ni mchezaji wa kwanza kufikisha pointi 20,000.

Baada ya kuibuliwa na timu ya Chuo Kikuu cha Louisiana (LSU), Pettit alisajiliwa na Milwaukee Hawks mwaka 1954.

Petit alistaafu kikapu mwaka 1965 akiwa na wastani wa kufunga pointi 26.4 na kucheza mipira iliyorudi [rebounds] mara 16.2 katika kila mchezo.

Related articles

Recent articles