16.7 C
New York

Hali tete ya usalama Ethiopia

Published:

ADDIS ABABA, Ethiopia

HALI ya kisiasa nchini Ethiopia inaibua uwezekano wa nchi hiyo kuingia kwenye vita. Mvutano kati ya Serikali na Chama kinachodhibiti Kaskani mwa Tigray, Tigray People’s Liberation Front [TPLF], umezidi kuibua hofu ya vita kutokea.

Katika kauli yake, Mshauri wa Waziri Mkuu, Getachew Reda, amesema wapiganaji wa TPLF wameshikilia viwanja wa ndege huko Tigray na kushambulia miji jirani ya Afar na Amhara.

“Inasikitisha kuona kwamba licha ya jitihada za wengi, ikiwamo jumuhiya ya kimataifa, katika kuepuka vita vingine mjini Tigray, uongozi wa TPLF umetekeleza mashambulizi mengine dhidi ya maeneo ya serikali huko Afar na Amhara,” alisema Getachew.

Getachew ambaye ni Mshauri wa Waziri Mkuu, Abiy Ahmed, aliwahi kuwa sehemu ya uongozi wa Tigray, kabla ya kukorofishana na TPLF mwaka 2025 na kuunga na Serikali.

Kabla ya kauli yake ya sasa, mamlaka za Tigray zililalamika kuwa vikosi vyao vimelazimishwa kuingia vitani. Ujumbe huo ulikuja baada ya ndege zisizo na rubani kushambulia maeneo ya Tigray.

Ni kutokana na mazingira hayo, wengi wanaiona Ethiopia ikielekea kwenye vita vilivyowahi kudumu kwa miaka miwili, kabla ya kufikia ukomo wake mwaka 2022.

Kwa mujibu wa wasuluhishi kutoka Umoja wa Afrika [AU], watu 600,000 walipoteza maisha, achilia mbali janga la njaa na wengi waliokimbia makazi yao.

Sasa, kwa miezi michache ya hivi karibuni, kumewapo na mvutano mkali kati ya Serikali na mamlaka za Tigray, huku kila upande ukiushutumu mwingine kwa kukiuka makubaliano ya amani.

Hivi karibuni, katika kile kilichoashiria hali mbaya zaidi, TPLF ilitangaza kuwaa imeungana na vikundi sita vya waasi kwa lengo la kuiondosha madarakani Serikali iliyoko madarakani mjini Addis Ababa.

Aidha, hatua ya wapiganaji wa Tigray kuteka viwanja vya ndege imesababisha Serikali ya Ethiopia kutangaza kusitisha safari zote za kwenda eneo hilo.

Related articles

Recent articles