16.7 C
New York

Utafiti: Tembo hujitibu wenyewe kwa mitishamba

Published:

Na mwandishi wetu, Gazetini

KWA mujiu wa utafiti wa Taasisi ya Mount Elgon, wanyama aina ya tembo hujitibu kwa mitishamba wanapopata wanapokabiliwa na magonjwa mbalimbali.

Aidha, utafiti huo ulioongozwa na wataalamu, akiwamo Dkt. Elodie Freymann kutoka Chuo Kikuu cha Brown cha Marekani, na kuchapishwa katika Jarida la Scientific Reports, umebaini kuwa tembo barani Afrika hutumia aina zaidi ya 35 ambayo ni tiba ya maradhi mbalimbali.

Moja ya miti iliyotajwa kwenye utafiti ni Angurweet, ukielezwa kutumiwa na tembo kwa ajili ya kukabiliana na maumivu ya tumbo.

Pia, Dkt. Freymann na watafiti wenzake walibaini kuwa tembo huchagua aina ya miti ya kutumia pindi wanapohisi maradhi.

Wakati huo huo, imeelezwa kupitia utafiti huo kwamba tembo wa kike ndiyo hufanya kazi ya kuwapa miti hiyo watoto wao wanapokuwa wanaumwa.

Wakizungumzia miti aina ya Angurweet, watafiti wanaeleza kuwa tembo wa kike [mama] hutafuna miti hiyo ili kulainisha, kabla ya kumpa mtoto wake anayeumwa.

Mmoja ya waliohojiwa katika utafiti huo, amesimulia alivyowahi kuona tembo wa kike akichanganya dawa hiyo na maziwa yake.

Kupitia video zilizonaswa kwa kamera zilizotegwa kwenye Mlima Elgon nchini Kenya, utafiti wa Taasisi hiyo umeeleza kuwa tembo wa eneo huvuna chumvi kwa ajili ya kuweka kwenye vyakula vyao.

Mwisho, historia ya tembo kujitibu kwa mitishamba ina miaka mingi. Mmoja ya waandishi wa vitabu, Claudius Aelian, aliwahi kueleza namna wanyama hao wanavyotumia mafuta ya miti ya mzaituni kujitibu majeraha.

Related articles

Recent articles