13.7 C
New York

Watu wenye wafuasi wengi zaidi Instagram

Published:

Na mwandishi wetu, Gazetini

KATI ya watu 20 wenye wafuasi [followers] wengi zaidi katika mtandao wa kijamii wa Instagram, 14 wanatoka nchini Marekani.

Hata hivyo, wanasoka wawili, Cristiano Ronaldo na Lionel Messi, ndiyo watu wenye ‘followers’ wengi zaidi katika mtandao huo ulioanzishwa miaka 16 iliyopita.

Ronaldo, raia wa Ureno anayekipiga katika klabu ya Al Nassr ya Saudi Arabia baada ya kuwika na Sporting Lisbon, Manchester United, Real Madrid na Juventus, ana wafuasi milioni 679.

Kwa upande wa Messi, Muargentina huyo aliyewahi kuwika Barcelona, PSG na sasa Inter Miami ya Marekani, ana wafuasi milioni 516, akiwa amezidiwa milioni 163 na mwenzake huyo.

Baada ya Ronaldo na Messi, anayefuata kwa kuwa na idadi kubwa ya followers huko Instagram ni mwanamuziki na mwigizaji raia wa Marekani, Selena Gomez. Bibiye huyo ana wafuasi milioni 403.

Katika nafasi ya nne ni mwigizaji mwingine wa Marekani, Dwayne Johnson, akiwa na wafuasi milioni 381, akifuatiwa na mtangazaji wa vipindi vya televisheni, Kylie Jenner [milioni 381].

Orodha hiyo inaye pia mke wa zamani wa Kanye West, Kim Kardashian, anayeshika nafasi ya saba kwa wafuasi milioni 344, akifuatiwa na Beyonce mwenye milioni 299.

Wengine ni Khloe Kardashian [milioni 291], Justin Bieber [milioni 286], Kendall Jenner [milioni 277], Taylor Swift [milioni 273], Virat Kohli milioni 272],
na Neymar [milioni 242].

Wanaofuata katika ‘Top 20’ ni Jennifer Lopez [milioni 240], Kourtney Kardashian [milioni 209], Miley Cyrus [milioni 205], Katy Perry [milioni 195], Zendaya [milioni 177], na Kevin Hart [milioni 172].

Related articles

Recent articles