26 C
New York

Kampuni za mafuta zinazonufaika vita vya Iran, Marekani

Published:

WASHINGTON DC, Marekani

FAIDA wakati wa vita. Ndicho kinachoonekana wakati huu Iran na Marekani zikiwa kwenye mgogoro unaotikisa si tu Mashariki ya Kati, bali dunia kwa ujumla.

Tangu vita hivyo vilipoanza, kisha Iran kufunga Mlango-Bahari wa Hormuz, baadhi ya kampuni za mafuta zimekuwa zikivuna faida ya mabilioni ya dola kutokanana na kupanda kwa bei ya nishati hiyo.

Bei ya mafuta imekuwa ikipanda kila Iran inapoufunga Mlango-Bahari huo unaopitisha meli zinazobeba asilimia 20 ya mafuta yanayoingia kwenye soko la dunia.

Inapotokea Hormuz kufungwa na soko la dunia kupata uhaba wa mafuta, bei huongezeka, hivyo kampuni zinazouza nishati hiyo kuendelea kupata faida mara dufu.

Moja ya kampuni zilizovuna faida kubwa wakati huu wa vita ni ExxonMobil ya Marekani. Imevuna faida ya Dola bilioni 14.5, ambayo ni kubwa zaidi kwa kipindi cha miaka minne ya hivi karibuni.

Kampuni ya pili kwa ukubwa nchini Marekani, Chevron, imepata faida ya Dola bilioni 12, kiasi ambacho haijawahi kuingiza kwa miaka sita iliyopita.

Shell ya Uingereza ni kampuni nyingine iliyonufaika na vita hivyo, ikielezwa kuingiza faida ya Dola bilioni 10 kwa kipindi hiki cha miezi mitano ya vita kati ya Marekani na Iran.

TotalEnergies ya Ufaransa nayo imevuna vya kutosha, ambapo faida yake kwenye biashara ya kuuza mafuta imeripotiwa kupanda kwa asilimia 67.

Aidha, kampuni ya BP ya Uingereza nayo imepata faida ya Dola bilioni 5.73 tangu vita vilipoanza Februari 28, 2026, mara mbili ya Dola bilioni 2.35 ilizovuna mwaka 2025.

Wakati huo huo, kampuni kubwa zaidi duniani kati ya zile zinazomilikiwa na Serikali, Saudi Aramco, imeiingiza Saudi Arabia faida ya Dola bilioni 32.69, sawa na ongezeko la asilimia 44.

Related articles

Recent articles