14.4 C
New York

Bayern yamfungia kazi Dani Olmo

Published:

MUNICH, Ujerumani

KLABU ya Bayern Munich imeripotiwa kuanza harakati za kuinasa saini ya winga wa Barcelona, Dani Olmo, ifikapo Januari, 2027.

Hatua ya Bayern kuanza kujipanga kwa ajili ya Olmo inakuja wakati huu mastaa wake wawili, Jamal Musiala na Michael Olise, wakiendelea kuhusishwa na klabu zingine.

Bayern imekuwa ikimtamani Olmo wa muda mrefu, tangu akiwa na RB Leipzig, kabla ya kuikataa ofa yao na kutimkia Barcelona.

Olmo aliyeibuliwa na Dinamo Zagreb, alifunga mabao 29 katika mechi 34 akiwa Leipzig, kabla ya Barcelona kumsajili kwa Pauni milioni 47 mwaka 2024.

Kwa miaka yake miwili ndani ya Camp Nou, mshambuliaji huyo ameweza kufunga mabao 20 na kutoa asisti 20 katika mechi zaidi ya 100.

Kwa sasa, thamani yake sokoni ni Pauni milioni 60. Olmo amefunga mabao 12 katika mechi 58 alizocheza katika kikosi cha timu yake ya Taifa ya Hispania.

Related articles

Recent articles