14.4 C
New York

Deco: Barcelona hatuna mpango na Gabriel

Published:

CATALUNYA, Hispania

MKURUGENZI wa ufundi wa Barcelona, Deco, ameweka wazi kuwa klabu hiyo haina mpango wa kumsajili kinda wa Manchester United, JJ Gabriel.

Gabriel [15], anahusishwa na klabu kubwa za Ulaya, zikiwamo Barcelona, Real Madrid, Bayern Munich na PSG.

“Hakuna cha kusema kuhusu kijana huyo,” amesema Deco na kuongeza: “Ni kawaida yetu kuhusishwa na wachezaji. Kwa sasa, hatuna mpango na mchezaji yeyote. Sina uhakika kama kuna kitu kitatokea na kwa kuwa ni mchezaji wa Manchester United, hatuhusiki naye.”

Gabriel hajafanya mazoezi na Man United tangu alipopachika ‘hat-trick’ katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa ya Vijana [Septemba 10, 2026].

Hata hivyo, kwa mujibu wa sheria, kinda huyo hatoruhusiwa kuitumikia klabu yoyote zaidi ya Man United kwa msimu huu wa 2026-27.

Related articles

Recent articles