24.4 C
New York

Wawili wafariki ajali ya helikopta

Published:

ATHENS, Ugiriki

AJALI ya helikopta mbili za kukabiliana na majanga ya moto zilizogongana nchini Ugiriki imesababisha vifo vya wafanyakazi wake wawili.

Katika ajali hiyo iliyotokea wakati wa zoezi la kuzima moto, waliopoteza maisha ni rubani raia wa Denmark na ofisa wa zima moto wa Ugiriki.

Wakati huo huo, taarifa juu ya tukio hilo zinaeleza kwa kina, kwamba rubani mwingine raia wa Uingereza na mratibu wa helikopta nyingine raia wa Ugiriki walisalimika.

Taarifa zinaeleza kuwa ajali hiyo ilitokea umbali wa kilometa 65 huko Magharibi mwa Mji Mkuu wa Athens.

Kwa upande wake, Waziri Mkuu wa Ugiriki, Kyriakos Mitsotakis, ametumia ukurasa wake wa X (zamani Twittwer) kueleza kusikitishwa kwake na tukio hilo.

Related articles

Recent articles