28.4 C
New York

Wanasiasa wamnyima kibarua kocha Italia

Published:

MILAN, Italia

ANDREA Pirlo amesema hawezi tena kupewa kibarua cha kuinoa timu ya soka ya Taifa ya Italia. Hiyo imesababishwa na wanasiasa.

Iko hivi; Pirlo ni miongoni mwa makocha wanahusishwa na kazi hiyo na hivi karibuni imeelezwa kuwa ndiye anayepewa nafasi kubwa.

Hata hivyo, wanasiasa nchini Italia wamesema mkongwe huyo wa soka hapaswi kupewa timu yao ya taifa kwa kuwa ana uhusiano na kampuni ya ‘kubeti’ ya Fonbet ya nchini Urusi.

Pirlo (47), alitangazwa kuwa balozi wa kampuni hiyo Oktoba, 2025, jambo ambalo wanasiasa wa Italia walilipinga.

Itakumbukwa kuwa Urusi haiungwi mkono na mataifa mengi ya Ulaya yaliyokerwa na hatua ya nchi hiyo kuivamia Ukraine mwaka 2022.

“Yeyote ambaye amekuwa akiiunga mkono Urusi baada ya mwaka 2022 hapaswi kupewa nafasi ya Serikali,” amesema mwanasiasa wa Chama cha Azione, Carlo Calenda.

Related articles

Recent articles